Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yawezesha wakimbizi wa Nigeria walioko Chad

UNHCR yawezesha wakimbizi wa Nigeria walioko Chad

Kulingana na takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, zaidi ya wakimbizi 5,000 kutoka Nigeria wameweza kupata hifadhi katika kambi ya Dar es Salam nchini Chad, iliyoko karibu na ziwa la Chad baada ya kukimbia vurugu za kutisha mwezi Disemba mwaka 2014. Jumla ya watu milioni 2.4 katika eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria, Cameroon, Chad na Niger wamepoteza makazi yao kufuatia mashambulizi ya Boko Haram. Katika Makala hii tunakutana na Bwana Hawali Oumar, ambaye ni mmoja wa wakimbizi waliopata matumaini baada ya kupata vifaa vya kuwasadia kwa uvuvi. Ungana na Selina Jerobon kwa undani Zaidi…