Tusilaumu mabadiliko ya tabianchi kwa baa la njaa Sudan Kusini- Shearer

22 Februari 2017

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa ujumbe wa umoja huo nchini Sudan Kusini, UNMISS, David Shearer amesema uhaba wa chakula nchini humo ni janga lililosababishwa na binadamu na si mabadiliko ya tabianchi au ukame.

Akizunguzma na waandishi wa habari kwenye mji mkuu Juba hii leo, Bwana Shearer amesema ziara yake kwenye majimbo ya Unity na maeneo ya Leer imemthibitishia hali hiyo.

Amesema sasa jambo muhimu ni suluhu ya kisiasa kwenye mzozo wa Sudan Kusini ulioanza miaka mitatu iliyopita akiangazia pia mjadala wa kitaifa utakaoanza mapema mwezi ujao,.

(Sauti ya Shearer)

“Nadhani jambo muhimu kwetu ni kuhakikisha mjadala wa kitaifa unakuwa shirikishi, ikimaanisha kuwa tunataka kuona pande nyingi zaidi zikishiriki. Iwapo tutakuwa wakweli na dhati kwenye kusaka amani, na hatimaye maridhiano yawepo basi tunaweza kueneza mashauriano hayo maeneo mengi.”

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter