Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Israel yaaswa kuheshimu sheria za kimataifa-OCHA

Israel yaaswa kuheshimu sheria za kimataifa-OCHA

Mratibu wa misaada ya kibinadamu na shughuli za maendeleo za Umoja wa Mataifa kwenye eneo la Wapalestina linalokaliwa Robert Piper, na mkurugenzi wa operesheni za shirika la Umoja wa mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA  kwenye Ukingo wa Magharibi Scott Anderson, wqmefanya ziara kwenye eneo la Mashariki mwa Jerusalem.

Eneo la Khan al Ahmar ni moja ya maeneo yenye jamii zenye dhidi Ukingo wa Magharibi zinazohaha kukidhi mahitaji ya lazima ya kila siku huku kukiwa na shinikizo kubwa kutoka kwa mamlaka ya Israel likiwataka kuondoka kwenye maeneo mengine waliyotengewa. Bwana Piper amesema hali hiyo haikubaliki na lazima ikomeshwe.

Ameongeza kuwa amri ya Israel ya kutaka kubomolewa kwa takriban makazi 140 ya jamii hiyo itaathiri makazi na maisha ya zaidi ya wakimbizi 140 na zaidi ya nusu yao ni watoto.

Majengo hayo yanajumuisha pia shule ya msingi ambayo inatoa elimu kwa takriban watoto 170. Piper ametoa wito kwa serikali ya Israel kuheshimu sheria za kimataifa za haki za binadamu na kutotekeleza bomoabomoa