Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wafunzeni watoto lugha za mama watambue utamaduni-Profesa Almeida

Wafunzeni watoto lugha za mama watambue utamaduni-Profesa Almeida

Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya lugha ya mama, imeelezwa kuwa kutojihusha na lugha hiyo kunaweza kumtenga mtu na utamaduni wa jamii yake.

Katika mahojiano na redio ya Umoja wa Mataifa kuhusu umuhimu wa lugha ya mama, mtafiti kutoka Brazil ambaye ni mhadhiri wa chuo kikuu cha New York mjini Abu Dhabi, Profesa Diogo Almeida amesema ni muhimu kujifunza lugha ya mama kabla ya kupevuka kwani akili ya mtoto ina uwezo wa kufanya hivyo, akisisitiza kuwa kuchelewa kunaweza kuleta ugumu katika kujifunza.

Kuhusu matumizi ya lugha mbalimbali katika utawandawazi amesema ni katika dunia ambayo imekuwa ndogo, ni muhimu kujua lugha za kimataifa kama vile Kiingereza lakini akatoa angalizo.

( Sauti Almeida)

‘Pamoja na kwamba kuwa njia ya mawasilaino ambayo inatumika dunia nzima ni kitu chema kwakuwa ni jambo la kinadharia, kuna hatari kubwa kwa lugha nyingine kutoweka na hivyo itasababisha kupotea kwa tofauti za kibinadamu.’’