Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto 65,000 wanaotumikishwa vitani waachiliwa-UNICEF

Watoto 65,000 wanaotumikishwa vitani waachiliwa-UNICEF

Takribani watoto 65,000 wameachiliwa kutoka katika vikosi vyenye silaha katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kupitia viongozi mbalimbali wa dunia wanaohuduhuria maadhimisho ya mkatabata wa Paris wa kukomesha matumizi ya watoto katika migogoro.

Miaka kumi iliyopita dunia ilitoa ahadi kwa watoto wanaotumikishwa vitani na kuchukua hatua iliyiosaidia watoto 65,000 kupta fursa mpya kwa maisha bora, imesema taarifa ya UNICEF ya leo ikimnukuu Mkurugnezi Mtendaji Anthony Lake.

Hata hivyo amesema mkutano wa leo hauhusu tu kutizama kilichotimizwa, bali pia kujikita mbele kwa ajili ya kazi iliyosalia ya usaidizi kwa watoto wanaotumikishwa vitani.

Kwa mujibu wa UNICFE, licha ya kwamba ni vigumu kupata idadi kamili ya watoto watumikishwao vitani kwasababu ya asili ya kuvunjwa kwa  sheria katika kuwatumikisha, shirika hilo linakadiria kuwa makumi elfu ya wavulana na wasichana walio chini ya umri wa miak 18 wanatumikishwa kote duniani.

Mathalani takwimu za shirika hilo la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto zinaonyesha kuwa nchini Jamhuri ya Afrika ya kati CAR, watoto takribani 17,000 wametumikishwa vitani, wengine 10,000 nchini Sudan Kusini, ilihali Nigeria ikikadiriwa kutumikisha watoto 2,000.