Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jumuiya ya kimataifa kuongeza msaada kwa bonde la ziwa Chad-O’Brien

Jumuiya ya kimataifa kuongeza msaada kwa bonde la ziwa Chad-O’Brien

Wiki hii Ijumaa Februari 24 jumuiya ya kimataifa inakutana Oslo Norway kujadili jinsi ya kuongeza msaada kwa bonde la ziwa Chad ambako nchi za Cameroon, Chad, Niger na Nigeria ziko katika hatihati ya janga kubwa.

Machafuko yakiwemo ya Boko Haram yamewafanya watu zaidi ya milioni 2.3 kuzihama nyumba zao huku milioni 7 wakikabiliwa na njaa. Utapia mlo uliokithiri unatishia maisha ya watoto zaidi ya nusu milioni huku jumla ya watu milioni 11 wakihitaji msaada wa haraka .

Akizungumzia matarajio katika mkutano huo wa Februari 24,  mratibu wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa Stephen O’Brien amesema

(CUT YA STEPHEN O’BRIEN)

“tumekadiria kwamba ili kukidhi mahitaji ya haraka tunahitaji dola bilioni 1.5 , na ni muhimu sana tunahitaji sasa kuwafikia watu na mahitaji yao ya lazima kwa ajili ya malazi, kwajili ya chakula , kwa ajili ya dawa , kwa ajili ya maji ya kunywa na kuhakikisha kwamba wana uwezo wa kujenga upya maisha yao baada ya kutawanywa na kutokuwa na nyumba za kurejea”