Kiir aahidi kuboresha uhusiano wake na UM

Kiir aahidi kuboresha uhusiano wake na UM

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, umesema kuwa Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir leo amekiri kwamba uhusiano baina ya serikali yake na Umoja wa Mataifa katika miaka mitatu iliyopita umekuwa na utata.

Rais Kiir amesema hayo wakati wa ufunguzi wa kikao cha pili cha Bunge la Serikali ya Mpito, akisema wakati umewadia sasa wa kuboresha uhusiano huo, na anatambua kuwa Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ni mwenye busara na hivyo akatoa ahadi....

(Sauti ya Kiir)

"Serikali yangu inatoa ahadi ya kufanya kazi kwa pamoja na kwa ukaribu zaidi naye ili kuboresha uhusiano wetu na wa mfumo wa Umoja wa Mataifa kwa ujumla."

Vile vile amesema uhusiano huo unamjumuisha pia mkuu mpya wa UNMISS, David Shearer kwani ana imani kuwa atashirikiana vyema na serikali ya Sudan Kusini ili kuboresha uhusiano huo.