Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lashtushwa na kifo cha Churkin

Baraza la usalama lashtushwa na kifo cha Churkin

Wajumbe wa baraza la usalama wameshtushwa na kifo cha ghafla cha balozi Vitaly Churkin, mwanadiplomasia wa Urusi na balozi wa kudumu wa Urusi kwenye Umoja wa Mataifa kilichotokea asubuhi ya Februari 20 mwaka 2017.

Wajumbe wa baraza wanamuomboleza balozi huyo aliyehudumu kwa zaidi ya miaka 40 katika masuala ya kidiplomasia nchini Urusi na kuwa balozi kwenye Umoja wa mataifa kwa zaidi ya muongo mmoja. Jumanne ya Februari 21 angekuwa anasherehekea miaka 65 ya kuzaliwa kwake.

Wajumbe wa baraza wametuma salamu za rambirambi na pole zao kwa familia ya balozi Churkin, serikali na watu wa serikali ya shirikisho ya Urusi kwa msima huo mkubwa.