Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukame wazidi kutawanya maelfu Somalia-UNHCR

Ukame wazidi kutawanya maelfu Somalia-UNHCR

Ukame umetawanya zaidi ya watu 135,000 ndani ya Somalia kuanzia mwezi Novemba mwaka jana kwa mujibu wa takwimu zilizokusanywa na shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, baraza la wakimbizi la Norway na mashirika ya kijamii nchini Somalia.

UNHCR inasema hatua madhubuti na fedha za ufadhili vinahitajika haraka ili kuepuka baa la njaa na kujirudia kwa zahma ya 2011 ambapo watu 250,000 walikufa, na zaidi ya nusu wakiwa ni watoto wa chini ya miaka mitano.

Kwa mujibu wa uopngozi wa Puntland, familia zaidi ya 20,000 zimehamia jimbo la Bari na zaidi ya watu 1600 wanahitaji msaada wa haraka Kaskazini mwa mji wa Galkayo.