Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampeni ya chanjo ya polio nchini nzima yazinduliwa Yemen-WHO/UNICEF

Kampeni ya chanjo ya polio nchini nzima yazinduliwa Yemen-WHO/UNICEF

Kampeni ya chanjo ya polio kwa nchi nzima imezinduliwa Jumanne nchini Yemen na wizara ya afya ya nchi hiyo kwa msaada wa shirika la afya ulimwenguni WHO na la kuhudumia watoto UNICEF kwa lengo la kuwachanja watoto zaidi ya milioni tano walio na umri wa chini ya miaka mitano.

Zaidi ya wahudumu wa afya 40,000 wanashiriki kampeni hiyo ya siku tatu . Pia viongozi wa dini, maafisa wa serikali na waelimishaji wa afya wanachagiza msaada kwa ajili ya kufanikisha kampeni hiyo.

Kwa mujibu wa WHO na UNICEF makundi yaliyo katika hatari zaidi kama wakimbizi wa ndani na wakimbizi wengine watafikiwa na kampeni hiyo. Christian Lindmeire msemaji wa WHO anaeleza zaidi kuhusu kampeni hiyo.

(SAUTI YA CHRISTIAN LINDMEIER)

“Kampeni hiyo ilianza katika majimbo yote isipokuwa Sa’ada lililo Kaskazini magharibi ambako itafanyika wiki ijayo na itajumuisha pia utoaji chanjo dhidi ya surua kwa ajili ya mlipuko unaoshuhudiwa huko.”