Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baa la njaa lakumba Sudan kusini-FAO/UNICEF/WFP

Baa la njaa lakumba Sudan kusini-FAO/UNICEF/WFP

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaonya kwamba takriban watu milioni 5 wanahitaji haraka msaada wa chakula, kilimo na lishe nchini Sudan Kusini. Amina Hassan na taaria kamili.

(Taarifa ya Amina)

Mashirika hayo la chakula na kilimo FAO, la mpango wa chakula duniani WFP na la kuhudumia watoto UNICEF katika taarifa yao ya pamoja yamesema vita na kuporomoka kwa uchumi kumewaacha watu 100,000 wakikabiliwa na njaa katika baadhi ya sehemu za Sudan Kusini ambako baa la njaa limetangazwa rasmi leo Jumatatu, huku watu wengine milioni moja wakitajwa kuwa katika hatihati ya kukumbwa na baa hilo. Luca Russo ni afisa mshauri wa masuala ya mikakati wa FAO.

(SAUTI LUCA RUSSO)

“Tunatumai kwamba baada ya kutangazwa baa la njaa , serikali na pande kinzani watakubali kuruhusu fursa ya kibinadamu katika maeneo hayo ambayo itakuwa muhimu katika kufanya mambo mawili moja kusambaza msaada wa chakula ambao ni muhimu kwa watu kuishi, lakini wakati huohuo kuwasaidia watu hao kurejesha maisha yao upya ili waweze kuishi.”

Yameongeza kuwa endapo msaada utawasili haraka basi hali ya njaa itadhibitiwa katika miezi ijayo. Idadi ya watu wasio na uhakika wa chjakula inatarajiwa kuongezeka hadi milioni 5.5 ifikapo msimu wa muambo mwezi Julai edapo hakuna hatua zitakazochukuliwa kudhibi kuenea kwa mtafaruku huo wa ukosefu wa chakula.