Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mifumo ya taarifa ya kijiografia kutumika kudhibiti maji El Salvador-UNESCO

Mifumo ya taarifa ya kijiografia kutumika kudhibiti maji El Salvador-UNESCO

Mpango unaoshughulika na masuala ya udhibiti wa maji katika shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni,UNESCO kwa kushirikiana na Wizara ya mazingira na maliasili ya El Salvador inafanya  hii leo Jumatatu Februari 20, inafanya mafunzo juu ya maji kwa maafisa wake na wadau wanaohusiana na masuala ya maji hivi leo mjini San Salvador  nchini El Salvador, Amerika ya kati.

Kwenye taarifa yake UNESCO imesema Amerika ya Kati ina wakazi milioni 40 au asilimia 70% wanaishi katika pwani ya Pasifiki ambako asilimia 30% pekee ya rasilimali ya maji asilia hutumika. Kuimarisha uwezo wa kiufundi wa taasisi na vyombo vyenye uhifadhi wa rasilimali ya  maji ni muhimu kwa kuboresha udhibiti wa maji.

Mafunzo hayo yana lengo la kukuza rasilimali za kitaifa na watendaji na uwezo wao wa kiufundi kwa kutumia zana za kijiografia za GIS kwa ajili ya usimamizi wa rasilimali za maji.

Matumizi hayo yatasaidia wadau katika kubuni, kuratibu na kufanya maamuzi ya uhifadhi bora rasilimali za maji.

Njia imeandaliwa ili kuzisaidia nchi wanachama katika ufuatiliaji na utekelezaji wa maendeleo endelevu kwa lengo la "kuhakikisha upatikanaji na usimamizi endelevu wa maji na usafi kwa wote" ambalo ni lengo la SDG6.