Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani mashambulizi ya hivi karibuni ya kigaidi nchini Iraq

UM walaani mashambulizi ya hivi karibuni ya kigaidi nchini Iraq

[caption id="attachment_305773" align="alignleft" width="351"]hapanapaleiraq

Umoja wa Mataifa umelaani mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika kusini mwa Baghdad Februari 16 ambapo kikundi cha kigaidi cha ISIL kiijulikanacho pia kama Da'esh kimedai kuhusika.

Taarifa hiyo imemnukuu msemaji wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ikisema kuwa wiki hii imeshuhudia mfululizo wa uhalifu wa mauaji katika mji mkuu wa Iraq. Ametoa rambirambi za dhati kwa familia za wahanga, ikiwa ni pamoja na serikali na watu wa Iraq.

Ameongeza kuwa UM utaendelea kushikamana na watu wa Iraq katika kupinga majaribio ya kueneza hofu, vitisho na chuki na pia kuisaidia serikali na watu wa Iraq katika juhudi zao za kupambana na ugaidi na msimamo mkali, hasa kwa kujenga kuaminiana na kuelewana kwa njia ya mazungumzo ya amani na umoja.