Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dunia ienzi siku ya haki kwa kudumisha haki-UM

Dunia ienzi siku ya haki kwa kudumisha haki-UM

Umoja wa Mataifa umezitolea mwito serikali kote dunani kuienzi  siku ya haki ya kijamii duniani mnamo Februari 20,  kwa kuchukua hatua sasa kwa ajili ya jamii yanye usawa.

Kwa mujibu wa chapisho la wataalamu wawili wa umoja huo kuhusu haki za binadamu, kuhakikisha utu wa kibinadamu kwa kila mmoja kunahitaji sera timilifu za haki za kijamii kutekelezwa, sio tu ndani ya nchi bali pia kimataifa.

Wataalamu hao wamesema wanachama wote wa Umoja wa Mataifa wamejizatiti kudumisha amani na utu wa kibinadamu, kama ilivyoanishwa kwenye katiba ya umoja huo na hivyo ahadi hiyo inahitaji utekelezaji sasa kwa ajili ya mustakabali mwema wenye haki kuu ya kijamii.

Hili litasaidia nchi kuheshimu ahadi zao na kuanzisha mazingira mujarabu ambapo haki na heshima zaweza kuzingatiwa wameongeza wataalamu hao wa haki za binadamu.