Wakimbizi wa Sudan Kusini zaidi ya 4,800 wahamishiwa kambi ya Gambella, Ethiopia
Mama na wanae wapumzika baada ya kukimbia machafuko Sudan Kusini.([Picha:UNHCR/R.R.Thot)[/caption]Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM wiki hii limewasafirisha wakimbizi wa Sudan Kusini kutoka eneo pa Pagak kwenye mpaka wa Sudan Kusini na Ethiopia na na kuwapeleka kwenye kambi mpya ya wakimbizi ya Nguenyyiel jimbo la Gambella, Ethiopia, na kufanya idadi ya wakimbizi walioahamishwa kuanzia mwanzo wa mwaka huu kufikia 4,833.
Uhamisho huu wa karibuni ni sehemu ya operesheni za IOM za lengo la kuwahamisha wakimbizi wapya wa Sudan Kusini na kuwapeleka kwenye maeneo salama kwa mpangilio maalumu.
Timu ya wauguzi ya IOM iliambatana na wakimbizi hao huku ikiwapa huduma kama za maji ya kunywa na chakula wakati wa safari. Jumla ya mabasi 95 yakibeba jumla ya familia 1,446 yamehusika katika operesheni hiyo.