Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hii ni fursa ya kuokoa mustakhbali wa bahari-UM

Hii ni fursa ya kuokoa mustakhbali wa bahari-UM

mkutanobahariMkutano wa maandalizi kuhusu mustakhbali endelevu wa matumizi ya bahari na viumbe vya majini umemalizika leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Mkutano huu wa matayarisho ya mkutano mkubwa wa bahari utakaofanyika Juni umetoa fursa kwa nchi wanachama kujadili mambo muhimu ya kufanya kuhakikisha kizazi kijacho hakikumbwi na zahma bali matumaini kutokana na matunda ya bahari. Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa idara ya habari na mawasiliano DPI , Cristina Gallach ameketi chini na baadhi ya washiriki wa mkutano huo kujua yaliyojiri na matarajio akiwemo Rais wa kikao cha 71 cha baraza kuu Peter Thomson akisema wameliangalia suala la bahari kwa maslahi ya kizazi kijacho.

image
Rais wa kikao cha 71 cha baraza kuu Peter Thomson.(Picha:UM/Rick Bajornas)
(SAUTI PETER THOMSON)

“Tunaliangalia suala hili kwa mtazamo wa watoto wetu na wajukuu zetu watakaokuja baada yetu hivyo hii ni katika mustakhbali wa baadaye, ili waweze kufurahia matunda ya bahari kama ilivyokuwa kwetu sisi tulipokuwa wadogo.”

Mkutano huo pia umeliangalia suala la bahari na utimizaji wa malengo ya maendeleo endelevu au SDG’s. Wu Hongbo ni msaidizi wa Katibu Mkuu kwa aajili ya masuala ya kiuchumi na kijamii.

(SAUTI YA WU HONGBO)

image
Wu Hongbo msaidizi wa Katibu Mkuu kwa aajili ya masuala ya kiuchumi na kijamii.(Picha:UM/Manuel Elias)
“Wakati tunazungumzia lengo la SDG 14, tunazungumzia usafiri baharini, tunafikiria uvuvi wa samaki kwa ajili ya chakula , tunafikiria pia utalii, lakini hiyo haitoshi , afya ya bahari na mazingira mabaya ya matuzmizi yasiyo endelevu ya rasilimali za bahari yana athari za moja kwa moja za utekelezaji wa malengo mengine ya SDG’s”

Na kwa upande wa nchi wanachama ambazo zina jukumu kubwa la kuhakikisha mtazamo wa ulinzi wa mazxingira ya bahari unatekelezwa wana Imani kwamba kila tatizo lina suluhisho. Isabell Lövin ni naibu waziri mkuu wa Sweden.

(SAUTI YA ISABELLA)

image
Isabell Lövin ni naibu waziri mkuu wa Sweden.(Picha:UM/Manuel Elias)
“Kila matatizo tunayoyaona yanasuluhu , tunahitaji kubadilishana uzoevu tushirikishane matendo mazuri, na mkutano wa bahari utakuwa ni kituo cha kubadilishana uzoefu huo na ujuzi , pia kuhamisha teknolojia na kuzisaidia nchi zinazoendelea ili ziwe na uwezekano wa kubadili katika njia ambayo inahitajika kwa ajili ya bahari , kwa sababu bahari inatuunganisha sisi sote.”