Skip to main content

Mkutano wa dharura kukabiliana na wadudu na maradhi wahitimishwa Hararare-FAO

Mkutano wa dharura kukabiliana na wadudu na maradhi wahitimishwa Hararare-FAO

Mkutano wa dharura wa siku tatu kukabiliana na mlipuko wa wadudu na magonjwa ya kilimo Kusini mwa Afrika umehitimishwa leo mjini Harare Zimbabwe kwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo FAO.

Kanda hiyo imekubwa na mlipuko mpya wa magonjwa na mimea na mifugo ambayo yanatishia maisha ya sehemu kubwa ya watu ambao wanategemea kilimo ili kuishi.

FAO inasema eneo hilo pia liko katika tahadhari ya uwezekano wa mlipuko wa mafua ya avian ambayo yatari yamethibitishwa nchini Misri, Nigeria na Uganda. David Phiri mratibu wa kanda yya Kusini mwa Afrika wa FAO anafafanua zaidi kuhusu walichoafikiana kwenye mkutano huo

(SAUTI YA DAVID PHIRI)

“Athari kubwa ni wadudu aina moja ya viwavi jeshi , pia kuna ugonjwa unaoshambulia mahindi kwa mazao, na kwa upande wa mifugo tuna ugonjwa wa miguu na midomo na tuna kimeta haya tayari yanasababisha matatizo mengi kwenye ukanda huu na tunahofia kwamba homa ya mafua ya avian aina ya H5N8 ambayo hivi sasa imeshathibitishwa Uganda inashukiwa kuathiri nchi zingine mbili Afrika Mashariki na huneda inakuja Kusini kwa sababu ya ndege pori ambao huama mara kwa mara”