EU yasaidia miradi ya uhakika wa chakula Tanzania kupitia WFP

EU yasaidia miradi ya uhakika wa chakula Tanzania kupitia WFP

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa Chakula dunini (WFP) limepokea mchango wa Euro milioni 9.5 kutoka Umoja wa Ulaya (EU) kwa lengo la kuunga mkono mradi wenye thamani ya Euro milioni 24.5 wa kusaidia kukuza uhakika wa Chakula na lishe katika mikoa ya kati nchini Tanzania. Rosemary Musumba na ripoti kamili.

(Taarifa ya Rose)

Mradi unawalenga watu wapatao 40,000 na wakati huohuo ukichangia katika kupunguza utapiamlo katika wilaya za Bahi na Chamwino mkoani Dodoma na Ikungi na Singida Vijijini katika mkoa wa Singida.

Mchango wa EU umetangazwa leo wakati wa hafla ya kutia saini makubaliano  jijini Dar es Salaam Tanzania baina ya Dr. Mpoki Ulisubisya, Katibu Mkuu Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto wa Tanzania, Michael Dunford, Mwakilishi wa WFP Tanzania na Roeland Van De Geer, Mkuu wa Ubalozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania.