Redio yaangaza wakimbizi

15 Februari 2017

Redio ni zana ya aina yake, kwani ndio chombo pekee chenye uwezo wa kufikia wasikilizaji kwa upana, kwa urahisi na kwa bei nafuu ulimwenguni kote. Hutumika kupasha habari kwa jamii za watu walio katika mazingira magumu na duni, waliosoma na ambao hawajasoma na muhimu zaidi ni uwezo wake wa kutoa habari za dharura na kuokoa maisha ya wengi kwa haraka.

Makala ya Assumpta Massoi inaangazia redio na mchango wake kwa wakimbizi nchini Iraq, ungana naye.