Maendeleo vijijini ni wajibu wa kimaadili:IFAD

15 Februari 2017

Rais wa mfuko wa kimataifa wa ufadhili kwa ajili ya maendeleo ya kilimo IFAD Bwana Kanayo F Nwanze amesema maendeleo vijijini ni wajibu wa kimaadili akioongeza kuwa watu wanapokabiliwa na hali ya uhai au kifo basi hakuna linatakowazuia kukimbia

(NWANZE CUT)

“Wakati watu wanakabiliwa na matarajio ya kufa kwa umasikini au njaa wanahama,. Wanahamia mijini , maeneo yaliyoendelea n ahata kwingineko. Kwao hakuna bahari iliyo pana zaidi, hakuna uzio ulio mrefu zaidi na hakuna mpaka uliodhibitiwa zaidi kuwafanya kina mama hao, waoto na wanaume walio na hamasa wasipite.”

Nwanze ameyasema hayo kwenye ufunguzi wa kikao cha baraza la 40 la utawala wa IFAD  ambako ametoa ombi lake la mwisho kwa serikali kuhakikisha zinafadhili maendeleo vijijini kabla muhula wa utawala wake kumalizika Machi 31 mwaka huu.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud