Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yakomboa maisha ya wakimbizi Al-Mokha

WHO yakomboa maisha ya wakimbizi Al-Mokha

Zaidi ya raia 8,000 wengi wao wanawake, watoto na wazee wamekimbia makazi yao wakati mgogoro ukishika kasi mjini Al-Mokha katika jimbo la Taizz nchini Yemen, imesema Shirika la Afya duniani WHO.

WHO inasema raia hao ghafla wamejikuta bila ya malazi na huduma za afya na wengi wao wamo katika hali mbaya.

Akihojiwa na redio ya Umoja wa Mataifa msemaji wa WHO mjini Sanaa, Yemen Tarik Jašarević anasema kuwa…

(Sauti ya cut 1 Jašarević)

"Tunakadiria kuwa zaidi ya raia million 14 hawana huduma sahihi za afya, mambo yanazidi kuwa mabaya zaidi, wafanyi kazi wa huduma za afya hawajalipwa na hawawezi kuendelea kufanya kazi yao na hii inapunguza zaidi huduma hizo, kuna upungufu wa madawa na mapigano yanazidi."

Amesema idadi ya wakimbizi wa ndani imeongezeka na hivyo inafanya kazi kwa kasi ili kukidhi mahitaji yao …

(Sauti ya cut 2 Jašarević)

"WHO inatumia timu 28 na magari kutoa huduma za msingi na afya kwa haraka kwenye majimbo 11. Pia kumekuwa na kipindupindu japokuwa watu waliougua si wengi imetubidi kuanzisha vituo 26 vya kutibu ugonjwa wa kuhara, kumekuwa na kesi za malaria na homa ya dengue katika pande za pwani, na cha muhimu ni kwamba huduma za afya ziko vibaya mno, chanjo imekuwa chini ya asilimia 25% "

WHO pia imesaidia vituo ambavyo havijaathirika zaidi kwa kuwapa dawa na vifaa vya afya ili kuhakikisha huduma za msingi kwa walengwa 20,000 kwa miezi 3.