Vijana wasivunjike moyo Sudan Kusini-Whitaker

14 Februari 2017

Balozi mwema wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO kuhusu amani na maridhiano, Forest Whitaker ametoa wito kwa vijana wa Sudan Kusini kusalia katika njia ya kimaadili wakitafuta amani.

Whitaker ambaye yumo ziarani nchini humo kutathmini mendeleo ya mpango wake kwa ajili ya vijana aliouzindua mwaka 2014 WPDI, amesema umewawezesha vijana kufundisha vijana wenzao ujuzi katika ujenzi wa amani, utatuzi wa migogoro na upatanishi, ujasiriamali na ufahamu wa kompyuta.

Amesema anawasiwasi mkubwa na matumaini ya vijana pindi vita vipya vikianza mara kwa mara na akawakumbusha vijana kuwa wao ndio matumaini ya sasa na baadaye nchini humo, hivyo akatoa wito kuhusu amani..

(Sauti ya Whitaker)

“Ikiwa tutasalia katika njia ya kimaadili, njia safi, na njia ya ukweli hatimaye uzito wake utaegemea upande wa amani, uhuru na haki"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud