Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uzalishaji nishati kwa samadi wabadili maisha Misri-ILO

Uzalishaji nishati kwa samadi wabadili maisha Misri-ILO

Nchini Misri uzalishaji wa nishati mbadala kwa kutumia samadi yameokoa wakazi wa mji wa Port Said ambao walikuwa wanahaha kupata gesi kwa ajili ya matumizi ya majumbani.

Mkurugenzi wa ILO ofisi ya Cairo, Misri Peter van Rooij amesema mradi huo ulioanza kwa majaribio kwenye mkoa huo wa Port Said unahusisha ukusanyaji wa samadi ambayo huwekwa kwenye mtambo na hatimaye kuzalisha gesi na mabaki yake kutumika mbolea mashambani.

Bwana Rooji amesema kwa nchi kama Misri ambayo ina idadi kubwa ya mifugo, nishati itokanayo na samadi husaidia kuhifadhi mazingira na pia kutatua uchafuzi wa mazingira.

Mmoja wa wanufaika, El Desouky Refaat amesema kwa mitambo yake ya kuzalisha nishati humpatia sawa na mitungi miwili ya gesi kwa mwezi na zaidi ya hapo mabaki ya mtamboni ni mbole nzuri inayoua wadudu mashambani.

Serikali ya Misri imesema ni matumaini yake kuwa mradi huo wa majaribio utaenezwa maeneo mengine ili manufaa yake yaenee kwa wananchi wengi zaidi.