Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukame wapandisha bei ya vyakula Afrika Mashariki:FAO

Ukame wapandisha bei ya vyakula Afrika Mashariki:FAO

Kwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo FAO ukame umesababisha kupanda kwa kasi bei ya vyakula katika mataifa ya Afrika Mashariki.

Katika takwimu za karibuni za uangalizi na ufuatiliani wa bei za vyakula wa shirika hilo zinaonyesha kwamba bei za Mahindi, mtama na nafaka zingine ziko katika bei ya juu sana au zimevunja rekodi hasa katika nchi za Ethiopia, Kenya, Somalia, Sudan Kusini , Uganda na Tanzania. Kama anavyofafanua Mario Zappacosta ni mtaalamu wa masuala ya uchumi wa FAO

(SAUTI YA MARIO)

“Sababu kubwa ya mtafaruku wa sasa ambao umeathiri karibu nchi nyingi za kanda ya Afrika Mashariki ni ukame, ukame ambao umeghubika eneo la Kusini mwa kanda hiyo kati ya mwezi Oktoba na Desemba. Lakini katika baadhi ya nchi mtafaruko umechangiwa pia na sababu nyingine kama vile vita na machafuko katika maeneo ya Sudan kusini na Somalia.”