Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zanzibar yafungua mahakama ya mtoto

Zanzibar yafungua mahakama ya mtoto

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF limesema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika ulinzi wa watoto baada ya kufungua mahakama mpya kwa ajili ya ulinzi wa watoto.

Mahakama hiyo ni ya tatu kufunguliwa Zanzibar na hutumika kusikiliza na kutoa hukumu za kesi kati ya familia na mtoto, mtoto mtukutu, mtoto na mtu mzima na kesi zingine za watoto wenye umri wa chini ya miaka 18.

Mtaalamu wa masuala ya hifadhi ya mtoto wa UNICEF Zanzibar, Bwana Ahmed Rashid Ali ameiambia idhaa hii kile kilichosababisha kuanzishwa kwa mahakama hiyo..

(Sauti ya Ahmed