Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanachama UM waimarishe ushirika kulinda mioundombinu dhidi ya ugaidi

Wanachama UM waimarishe ushirika kulinda mioundombinu dhidi ya ugaidi

Ushirikiano wa kukabiliana na ugaidi baina ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ili kulinda miundombinu ni muhimu na unahitaji kuwa mpana zaidi, kwa mujibu wa afisa mwandamizi wa umoja wa Mataifa.

Ameyasema hayo mkuu wa baraza la utawala wa Umoja wa Mataifa Maria Luiza Ribiero, wakati wa kura ya bila kupinga kupitisha azimio hilo jumatatu.

Azimio hilo lina lengo la kuimarisha jukumu la kimataifa dhidi ya mashambulizi ya kigaidi kwenye huduma za umma kama vile nishati, na mitambo ya maji. Bi Ribiero amelipongeza baraza la usalama kwa kujikita na suala hilo wakati huu ambapo tishio la ugaidi limetamalaki kote ulimwenguni

(SAUTI YA MARIA RIBIERO)

“Hulka ya ugaidi wa kimataifa inahitaji juhudi za pamoja zilizoratibiwa na nchi na wadau wote wa kimataifa, hata hivyo tunahitaji kukiri kwamba juhudi za ushirikiano wa kimataifa kupambana na ugaidi zimekuwa ndogo, hususani katika masuala ya miundombinu muhimu. Kimkakati hii inamaanisha kwamba jumuiya ya kimataifa inahitaji kuungana na kuwa wabunifu zaidi, na watendaji zaidi ikiwa ni pamoja na kujenga ushirika imara biana ya sekta za umma na binafsi”

Naye Jugen Stock katibu mkuu wa shirika la polisi wa kimataifa INTERPOL lililo na jukumu kubwa la kukabiliana na changamoto hiyio ya ugaidi akihutubia baraza la usalama kwa njia ya video ameainisha baadhi ya binu zinazopaswa kuchukuliwa na serikali na mashirika ili kujiandaa na uwezekano wa shambulio la kigaidi ikiwemo kutumia ndege zisizo na rubani au drones

(SAUTI YA JUGEN)

“hivyo ni jinsi gani tunaweza kujiandaa kukabiliana na tishio hilo kwa miundombinu yetu , jibu fupi ni kuwawwezesha wadau wote kuweza kuwa tayari kujiandaa, kuweza kuzuia na kukabiliana na mashambulizi kama hayo.”

Ameongeza kuwa ubadilishanaji wa taarifa kuhusu masuala ya ugaidi umeimarika lakini akaunga mkono wito wa baraza wa kutaba kuboresha zaidi juhudi za kimataifa kupambana na uhalifu huo.