Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres alaani uvurumishaji wa kombora DPRK

Guterres alaani uvurumishaji wa kombora DPRK

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amelaani vikali hatua ya serikali ya Jamhuri ya watu wa Korea au DPRK kurusha kombora la ballistic.

Nchi hiyo ambayo pia inajulikana kama Korea Kaskazini, imearifiwa kufanya majaribio ya kombora la masafa ya kati siku ya Jumapili. Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wake Jumatatu, Bwana Guterres ameliita jaribio hilo kuwa ni ukiukwaji mwingine wa maazimio ya baraza la usalama unaofanywa na serikali ya DPRK.

Baraza la usalama linakutana baadaye hii leo kwa faragha kujadili suala hilo. Bwana Guterres amesema uongozi wa DPRK ni lazima urejee kutekeleza wajibu wake wa kimataifa na kufuata njia ya kuachana na nyuklia.