Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM na wadau watoa ombi la mamilioni ya dola kwa ajili ya DR Congo

UM na wadau watoa ombi la mamilioni ya dola kwa ajili ya DR Congo

Umoja wa Mataifa na washirika wake wa masuala ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, wametoa ombi la karibu dola milioni 750 ili kuwasaidia watu milioni sita nukta saba mwaka huu nchini humo.

Akizungumzia umuhimu wa ombi hilo Rein Paulsen mkuu wa ofiri ya kuratibu masuala ya kibinadamu nchini DRC (OCHA) amesema ni muhimu sana kwa dunia kutosahau uhahara wa mahitaji ya kibinadamu nchini humo.

Ombi la mwaka 2017 ni dola milioni 748 , kama sehemu ya mpango wa miaka mitatu wa kuchukua hatua dhidi ya mahitaji ya kibinadamu kwa mamilioni ya raia walioathirika na moja ya migogoro ya muda mrefu duniani.

Mpango huo wa hatua wa miaka mitatu umeandaliwa na mfumo wa Umoja wa Mataifa, Benki ya dunia na washirika wengine.