Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dola bilioni 1.6 zahitajika kukidhi mahitaji Sudan Kusini:OCHA

Dola bilioni 1.6 zahitajika kukidhi mahitaji Sudan Kusini:OCHA

Mashirika ya misaada ya kibinadamu yametoa ombi la dola bilioni 1.6 ili kutoa msaada wa kibinadamu wa kuokoa maisha ya na ulinzi kwa watu milioni 5.8 Sudan Kusini kwa mwaka 2017.

Kwa mujibu wa mratibu wa shirika la masuala ya kibinadmu OCHA nchjini Sudan kusini Eugene Owusu , hali ya kibinadamu nchini humo inaendelea kudorora kutokana na mchanganyiko wa mambo imewemo vita, kuporomoka kwa uchumi na mabaddiliko ya tabia nchi.

Ameongeza kuwa mahitaji ya watu yataongezeka hasa katika msimu ujao wa muambo.

Mashirika ya misaada yanakadiria kuwa takribani watu milioni saba unusu kote Sudan Kusini hivi sasa wanahitaji msaada wa kibinadamu na ulinzi.