Skip to main content

Tuimarishe ushirikiano ili kukidhi mahitaji ya kibinadamu: Guterres

Tuimarishe ushirikiano ili kukidhi mahitaji ya kibinadamu: Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema ushirikiano kati ya mashirika ya kibinadamu duniani ni muhimu katika kukidhi mahitaji ya kibinadamu duniani.

Bwana Guterres amesema hayo alipotembelea leo kituo cha kutoa misaada ya kibinadamu cha Mfalme Salman mjini Riyadh nchini Saudi Arabia, kituo ambacho amesema alishuhudia kikianzishwa akiwa Kamishna Mkuu wa wakimbizi na sasa kinaendeleza kutoa usaidizi wa kiutu si tu Yemen na Syria bali pia kwingineko duniani.

Amewatakia kila la heri na mafanikio katika kusaidia watu wengi walio katika dhiki na mahitaji duniani akisema Umoja wa Mataifa pekee hauwezi kukidhi mahitaji hivyo ubit ndio kitu muhimu.

Akiwa nchini Saudia Arabia Katibu mkuu amekutana na viongozi mbali mbali akiwemo Mfalme na viongozi wengine waandamizi.

Atatembelea pia falme za kiarabu, Oman, Qatar na Misri.