Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Simulizi za hamasa UM ukienzi siku ya kimataifa ya wanawake katika sayansi

Simulizi za hamasa UM ukienzi siku ya kimataifa ya wanawake katika sayansi

Tayla Ozdemir. Picha: UN Photo/Eskinder DebebeBaraza kuu la Umoja wa Mataifa limekuwa na tukio maalum la kuadihimisha siku ya kimataifa ya wanawake na wasichana ikiadhimishwa kesho Februari 11, likijadili mada kadhaa ikiwamo Jinsia, sayansi na maendeleo endelevu.

Umuhimu wa vyombo vya habari  na kuchukua hatua kutoka maono hadi vitendo ni miongoni mwa mada zilizojadiliwa katika mkutano huo ulioandaliwa na ubalozi wa Malta katiak Umoja wa Mataifa na  taasisi  ya kimataifa ya sayansi, RASIT.

Akihutubia mkutano huo, Bi Marie Paule Roudil  , mkurugenzi wa ofisi ya shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni  UNESCO, New York, Marekani  amesema dunia inahitaji sayansi na sayansi inahitaji wanawake  hivyo wakati umefika, kundi hilo lipigiwe chepuo na kupewa kipaumbele katika sayansi.

Msichana huyu Talya Ozdemir kutoka Uturuki aliamsha hisia za washiriki kwa kuhutubia mkutano huu akisema kuwa inasikitisha kwamba hata katika  tafiti mbalimbali na ugunduzi , wanasayansi wakike hawatajwi, jambo linalowanyima fursa wanasayansi chipukizi kwani wanakosa mtu wa mfano.

Hivyo amweshauri...

( Sauti Talia)

‘‘Nadhani tunahitaji habari chanya za vyombo vya habari kuhusu mafanikio ya wanawake katiak sayanasi, na pia tufundishwe kuhusu wanawake na sayansi mashuleni. Sayansi ina jukumu muhimu katika maisha yetu ya kila siku kwani intaneti, komputa, dawa na hata usafiri  vyote vinategemea sayansi.’’

Wajumbe katika mkutano huo wamesimulia hadithi za hamasa kwa wanawake na wasichana kushiriki katika sayansi, changamoto na fursa.

Wachangiaji wengine wamesema  majidiliano kuhusu ushiriki wa wanawake na wasichana katika sayansi ni muhimu yaendelee katika jamii, wakisema kuwa hamasa hiyo inaweza kuchochea shabaha kwa wasichana kushiriki kimkamlifu katika fani hiyo.