Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake hukatishwa ndoto zao za kuingia katika sayansi  mapema

Wanawake hukatishwa ndoto zao za kuingia katika sayansi  mapema

Wakati siku ya kimataifa ya wanawake na wasichana ikiadhimishwa kesho Februari 11, hii leo hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York kumefanyika tukio maalum la kuenzi siku hiyo inayopigia chepuo ushiriki wa kundi hilo katika sayansi. Joseph Msami na taarifa kamili.

( TAARIFA YA MSAMI)

Wadau mbalimbali wakiwamo Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya wanawake UN Women wamengazia namna wanawake na wasichana wanavyokatishwa ndoto zao utotoni kutokana na mitizamo hasi ya kijamii .

Katika muktadha huo, mjadala umejikita katika utafiti wa hivi karibuni unaoonyesha kuwa katika umri wa miaka sita, wasichana wanakosa ujasiri wa kueleza uwezo wao wa akili pamoja na kujiunga katikashuguli zinazohitaji uwezo mkubwa wa akili ikilinganishwa na wavulana.

Mapema juma hili , Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya anga za juu UNOOSA, imekuwa na mkutano mjini Vienna nchini Austria kujadili wanawake mashuhuri walioshamiri katika masuala ya anga, ambapo Mkurugenzi wa ofisi hiyo Simonetta Di Pippo ametaja changamoto katika kutimiza shabaha hiyo.

( Sauti Di Pippo)

‘‘Wakati wanadamu wakifanya mabadiliko makubwa ya sanyasi na teknolojia, bado kuna ukosefu mkubwa wa usawa wa kijinsia katika tasinia ya sayansi, teknolojia, uhandisi na mahesabu. Wakati kuna hamasa ya kusonga mbele, mchango wa wanawake na umuhimu wao bado hautumiwi ipasavyo. Inasikitisha kwamba katika karne ya 21, katika fani zifahamikazo kwa kuvunja mipaka, bado hatutumii vyema uwezo wa wanawake.’’