Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana Sudan Kusini wadai amani mwaka huu 2017

Vijana Sudan Kusini wadai amani mwaka huu 2017

Vijana nchini Sudan Kusini wameanzisha kampeni kupitia vyombo vya habari ili kupaza sauti ya amani, wakitaka serikali na pande husika katika mapigano kusitisha umwagaji damu nchini humo mwaka huu wa 2017.

Kampeni hiyo inakuja wakati Umoja wa Mataifa unasema idadi ya raia waliokimbia nchini humo tangu kuanza machafuko mwaka 2013 imevuka milioni 1.5 ilhali wakimbizi wa ndani ni milioni 2.1.

Akihojiwa na Radio Miraya ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, Ayak Chjol Deng wa Kundi la Utetezi wa Vijana, amesema vijana wanataka jamii za kikanda na za kimataifa, kuweka shinikizo zaidi kwa wadau husika kusitisha mapigano haraka, akigusia kampeni ya Umoja wa Afrika ya "Nyamazisha Silaha 2020" ...

(Sauti ya Ayak)

"Hatuwezi kusubiri hadi mwaka 2020 kunyamazisha silaha, tunataka zinyamaze hata jana. Tunafanya kampeni kwa ajili ya sitisho la mapigano iliyo aminifu na ya ukweli , tunataka kuona wadau wote wanahusika, hasa vijana,"