Skip to main content

GAVI yaombwa kuwezesha utoaji wa chanjo ya HPV Tanzania

GAVI yaombwa kuwezesha utoaji wa chanjo ya HPV Tanzania

Shirika la afya duniani, WHO kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania wamewasilisha ombi kwa ubia wa chanjo duniani, GAVI ili kufanikisha utoaji wa chanjo dhidi ya kirusi cha Humani Papiloma, HPV kinachosababisha saratani ya shingo ya kizazi. Taarifa zaidi na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Dkt. Alphoncina Nanai ambaye ni afisa wa WHO anayehusika na magonjwa yasiyopatiwa kipaumbele, NTD nchini Tanzania, ameiambia Idhaa hii kuwa ombi hilo linafuatia mafanikio ya majaribio ya chanjo hiyo kwenye mkoa wa Kilimanjaro miaka miwili iliyopita na ombi likikubaliwa matarajio ni kuanza kutoa chanjo hiyo nchi nzima mwaka 2018.

(Sauti ya Dkt. Alphoncina)

Amesema chanjo hiyo hutolewa mara mbili ambapo baada ya chanjo ya kwanza mtoto anatakiwa kurejea baada ya miezi sita kwa hiyo changamoto ambayo walibaini wakati wa majaribio ni mtoto kurejea.

(Sauti ya Dkt. Alphoncina)