Sauti zaidi zapaswa dhidi ya shambulio nchini Afghanistan
Katika taarifa yao, wanachama hao wametuma salamu za rambirambi kwa jamii za waliofariki na kwa watu na serikali ya Afghanistani na kuwatakia afueni ya haraka majeruhi.
Wanachama wameelezea wasiwasi wao wa vitisho vinavyotokana na makundi ya Taliban, Al-Qaida, ISIL au Da'esh na makundi mengine haramu yenye silaha dhidi ya raia, jeshi la kitaifa na usalama wa kimataifa nchini Afghanistan.
Wametaka wahusika wafikishwe mbele ya sheria huku wakisema hakuna jambo lolote linaloweza kuhalalisha ugaidi.
Nao ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA umelaani tukio hilo ambapo mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu nchini humo Tadamichi Yamamoto amesema kuwa shambulio hilo lilifanywa makusudi kuwalenga wafanyakazi wa mahakama walipokuwa wanaondoka Ofisini, akiutaja kuwa ukatili.