Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huu ni mwaka wa mabadiliko Libya: Kobler

Huu ni mwaka wa mabadiliko Libya: Kobler

Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya (UNSMIL), Martin Kobler, leo amelihutubia baraza la usalama akisema mwaka 2017 ni mwaka wa uamuzi kwa manufaa ya watu wa Libya.

Umoja wa Mataifa iliwezesha utiwaji saini wa makubaliano ya kisiasa LPA, mwezi Disemba mwaka 2015, yaliyokuwa na lengo la kuanzisha serikali ya umoja wa kitaifa, baada ya miaka kadhaa ya machafuko nchini humo.

Kobler amezungumza na redio ya Umoja wa Mataifa kabla ya kulihutubia baraza hilo ambapo amesema licha yamigawanyiko baina ya makundi ya kisiasa nchini Libya, kwa msaada wa jumuiya ya kimataifa, mwaka huu kunahitajika mabadiliko.

Ameeleza  ikiwa makubaliano ya mwaka 2015 yamepiga hatua hatua.

( Sauti Kobler)

‘’Makubaliano yaani LPA yalikuwa chombo muhimu katika kuitoa nchi kataika machafuko ya kisiasa, mwaka 2016 ulikuwa mwaka ambapo hali iliimarika. Sio ya kuridhisha, lakini anagalu iliimarika. Kulikuwa na kiwango kidogo cha machafuko.’’