Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IPU kuchunguza ukiukwaji wa haki za wabunge

IPU kuchunguza ukiukwaji wa haki za wabunge

Muungano wa mabunge duniani, IPU umesema una wasiwasi mkubwa juu ya ukiukwaji wa haki za wabunge ikiwemo kutoheshimu kinga ya za wabunge.

Kamati ya bunge hilo lenye kushughulikia visa 452 ulimwenguni kote hivi sasa limesema ukiukwaji huo ni pamoja na unyanyasaji, kutengwa katika ofisi kinyume na sheria, kufungwa jela, mateso na mauaji.

Wakati wa kikao chake cha mwezi uliopita, kamati hiyo imepitisha uamuzi kwa za wabunge 227 kutoka nchi 16, ambapo zaidi ya wabunge 100 walioathirika wanatoka Malaysia, Nicaragua na Uturuki, na hivi sasa imeamua kutuma wajumbe kuchunguza hali ya wabunge waliofungwa kizuizini nchini Uturuki.

Kamati hiyo pia imepitisha uamuzi wa visa kutoka Bahrain, Burundi, Iraq, Kuwait, Mongolia, Myanmar, Rwanda, Sri Lanka, Yemen na Zambia, na kukubali kuchunguza visa vingine kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, El Salvador na Venezuela