Skip to main content

Awamu ya pili ya uchaguzi wa Rais waendelea Somalia

Awamu ya pili ya uchaguzi wa Rais waendelea Somalia

Awamu ya pili ya uchaguzi wa Rais nchini Somalia unaendelea baada ya wagombea watatu kusalia huku mmoja akijiondoa katika kinyanga’nyiro hicho kinachowahusisha wabunge wa nchi hiyo.

Amnian Hassan na taarifa kamili.

(TAARIFAYA AMINA)

Matokeo ya awamu ya kwanza ya uchaguzi huo ambao unafanyika uwanja wa ndege kwa sabaabu za kiusalama, yametolewa ambapo wanaongoza hadi sasa ni, Hassan Sheikh Mohamud 88, Mohamed Farmajo 72, Sheikh Sharif 49, Omar Abdirashid Sharmarke 37.

Hata hivyo muda mfupi baada ya matokeo hayo mgombea Omar Abdirashid Sharmarke alijitoa na hivyo kupisha wagombea wengine watatu wanaochuana kwenye awamu ya pili ya uchaguzi.

Kwa mujibu wa matangazo ya moja kwa moja ya wavuti wa ujumbe wa Muungano wa Afrika nchini Somalia AMISOM, upigaji kura unafanyika bila tafraniyoyote.

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Michael Keating amesema uchaguzi huu ni muhimu na ikiwa kila kitu kitaenda sawa.

(Sauti ya Keating)

"Hii itakuwa mpito wa amani wa madaraka. Jambo muhimu zaidi ni kwamba rais mpya anakubaliwa kuwa amechaguliwa kisheria na umma kupitia wabung na ndiyo maana ni muhimu."

Jumla ya wapiga kura 239 wanashiriki katika mchakato huo.