Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Machafuko yanazidi Sudan Kusini, aonya Dieng

Machafuko yanazidi Sudan Kusini, aonya Dieng

Mshauri Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuzuia mauaji ya kimbari Adama Dieng ameelezea kusikitishwa kwake kufuatia kuendelea kwa machafuko katika maeneo kadhaa nchini Sudan Kusini.

Bwana Dieng katika taarifa hiileo, yake amesema licha ya Rais wa taifa hilo Salva Kiir kusaini na kuahidi kukomesha machafuko, bado machafuko yanaendelea katika maeneo mbalimbali na kwamba ghasia zaidi zinatarajiwa.

Amesema mchakato wa amani bado haujawezeshwa na usitishwaji kabisa wa mapigano, hatua inayozorotesha uwezekano majadiliano yaliyopendekezwa na serikali kutekelezwa.

Mshauri huyo maalum, mathalani amesikitishwa na hali katika eneo liitwalo Kajo-Keji, Kusini mwa Juba ambapo raia wamekimbia wakihofia machafuko.

Mwezi Januari pekee zaidi ya raia 52,000 wa Sudan Kusini walikimbilia Uganda, wakitokea Yei, Morobo, Lainya na Kajo-Keji