Skip to main content

Uchaguzi wa rais Somalia ni leo

Uchaguzi wa rais Somalia ni leo

Hatimaye uchaguzi wa rais nchini Somalia unafanyika leo ambapo wagombea 23 wanapigiwa kura na hivyo kuhitimisha mchakato wa uchaguzi nchini humo uliofanyika kwa miezi 18.

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Michael Keating amesema wagombea hao wote ni wanaume baada ya mgombea pekee mwanamke kujitoa kabla ya hatua ya kujiandikisha.

Wapigaji kura ni wabunge 329 wa bunge la juu na chini waliochaguliwa na wananchi na upigaji kura unafanyika katika uwanja wa ndege wa Mogadishu baada ya vituo vya awali vya kupigia kura kuhamishwa ili kufanikisha uchaguzi huru na haki.

(Sauti ya Keating)

“Iwapo mgombea yoyote anapata theluthi mbili ya kura katika awamu ya kwanza, huyo atakuwa Rais, ikishindikana wanaingia awamu ya pili kwa walioshika nafasi nne za juu, akikosa theluthi mbili wataingia awamu ya tatu na yeyote atakeyepata kura nyingi atakuwa Rais. Na ataapishwa mara moja mbele ya wabunge wote, wakuu wa jeshi, polisi na jamii ya kimataifa. ”

Na iwapo kila kitu kitaenda sawa…

(Sauti ya Keating)

“Hii itakuwa mpito wa amani wa madaraka. Jambo muhimu zaidi ni kwamba rais mpya anakubaliwa kuwa amechaguliwa kisheria na umma kupitia wabung na ndiyo maana ni muhimu.”