Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ISIL bado tishio, haturudi nyuma-Feltman

ISIL bado tishio, haturudi nyuma-Feltman

Baraza la usalama leo limekutana kwa ajili ya mashauriano kuhusu tishio la amani ya kimataifa na usalama linalosababishwa na kundi la kigaidi ISIL na washirika wake na juhudi za Umoja wa Mataifa katika kukabiliana na kundi hilo.

Mkuu wa masula ya siasa katika umoja huo Jeffrey Feltman amewasilisha ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu mkakati huo unaowezeshwa na nchi wanachama ambapo amesema ISIL bado ni tishio duniani ikiwemo barani Afrika hususani Magharibi mwa bara hilo.

(Sauti DFeltman)

‘ISIL imeongeza uwepo wake Magharibi mwa Afrika, washirika wake Boko Haram wanajaribu kusambaza ushawishi wao wa mashambulizi ya kigaidi nje ya Nigeria na kusalia tishio kubwa.’’

Amesema juhudi za kukabaliana na kundi hilo zinaendelea kuzaa matunda na zinasongeshwa mbele.

(Sauti Feltman)

‘Juhudi za kuimarisha uwezo wa nchi wanachama Afrika Mashariki na Magharibi zinaendelea ili kukabiliana na utekaji nyara ambao ni chanzo kikuu cha fedha kwa ISIL na washirika.’’