Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miaka 10 sasa bila mtoto wa kike au mwanamke kukeketewa Olepolos Kenya

Miaka 10 sasa bila mtoto wa kike au mwanamke kukeketewa Olepolos Kenya

Umoja wa Mataifa ukipigia debe hatua za kutokomeza ukeketaji dhidi ya watoto wa kike na wanawake kote ulimwenguni, nchini Kenya harakati zinazidi kushika kasi na hata kuna nuru kwani wakazi wa Olepolos katika nchi hiyo wa Afrika Mashariki hawajashika kiwembe kumkeketa mtoto wa kike au mwanamke kwa miaka kumi sasa. Je nini wamefanya nini? Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza kwa njia ya simu na Caroline Murgor, mratibu wa kitaifa wa mradi wa pamoja wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, na lile la idadi ya watu, UNFPA wa kutokomeza FGM nchini Kenya. Kwanza anaanza kwa kuelezea mbinu mbadala ya unyago isiyoambatana na ukeketeaji.