Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuondokane na mila hii inayowanyima utu wa wanawake- Guterres

Tuondokane na mila hii inayowanyima utu wa wanawake- Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametaka hatua zaidi dhidi ya ukeketaji watoto wa kike na wanawake.

Guterres amesema hayo katika ujumbe wake wa siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji duniani hii leo.

Amesema kitendo hicho cha kikatili ni ukiukaji wa haki za binadamu na pia kinawanyima wanawake na wasichana utu wao, huku ikihatarisha afya zao.

Bwana Guterres amesema machungu yatokanayo na FGM hudumu maisha na wakati mwingine husababisha vifo.

Kwa mantiki hiyo ametaka hatua duniani kufanikisha lengo la kutokomeza FGM kwa maslahi ya wanawake, wasichana, jamii na mustakhbali bora wa ulimwengu wote.