Saratani iligharimu dunia zaidi ya dola trilioni 1.6 mwaka 2010- WHO
Kuelekea siku ya saratani duniani tarehe Nne mwezi huu, Shirika la afya ulimwenguni, WHO limesema gharama zitokanazo na matibabu dhidi ya saratani ni kubwa kuliko zile za kinga na tiba wakati wa hatua za mwanzo za ugonjwa huo unaosababisha kifo cha mtu mmoja katika kila watu sita duniani kote. Joseph Msami na ripoti kamili.
(Taarifa ya Msami)
WHO imetolea mfano mwaka 2010 ambapo gharama za kiuchumi na kiafya zitokanazo na saratani ilikuwa dola trilioni 1.16 duniani kote.
Kwa mantkii hiyo ili kupunguza gharama, WHO inazindua mwongozo mpya wa kuwezesha nchi yoyote bila kujali kipato chake iweze kuimarisha ugunduzi wa saratani mapema.
Dkt. Alphoncina Nanai, Afisa mhusika wa magonjwa yasiyopatiwa kipaumbele, NTDs, WHO nchini Tanzania anasema mwongozo huo unalenga...
(Sauti ya Dkt. Nanai)
Wakati huo huo shirika la kimataifa la nishati ya atomiki, IAEA , limesema liko mstari wa mbele katika kukabili saratani kwenye nchi zinazoendelea.