Machafuko yasababisha vifo vya raia CAR, UM walaani

Machafuko yasababisha vifo vya raia CAR, UM walaani

Kuzuka kwa machafuko baina ya makundi mawili yenye silaha nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, kumesababisha madhila kwa raia ikiwemo vifo, majeraha na kufurushwa makwao na hivyo Umoja wa Mataifa umetaka kulindwa kwa raia na kuheshimiwa kwa sheria za kimataifa za kibinadamu. Rose Mary Musumba na taarifa kamili.

( TAARIFAYA ROSE)

Machafuko hayo yaliyoripotiwa kuzuka jana katika miji ya Bocaranga na Ouham jimboni Pende kumesababisha watu 9,000 ambao walihifadhiwa msituni kilometa 15 hadi 20 mwa miji hiyo , kusaka hifadhi katika maeneo mengine.

Kaimu Mratibu wa misaada ya kibinadamu nchini CAR, Dk Michel Yao amelaani mashambulizi dhidi ya raia na wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu, wakati huu ambapo majengo ya asasi za kiraia yameshambuliwa, kuchomwa moto na kuporwa.

Taarifa pia zimasema kuwa kanisa, maduka na masoko yamechomwa moto, kufuataia ghasia hizo.