Skip to main content

DRC imuenzi Tshisekedi kwa kutekeleza makubaliano ya kisiasa: MONUSCO

DRC imuenzi Tshisekedi kwa kutekeleza makubaliano ya kisiasa: MONUSCO

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja Mataifa na mkuu wa ujumbe wa Umoja huo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC Maman Sidikou ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha kiongozi wa upinzani nchini humo Etienne Tshisekedi, aliyefariki dunia Februari mosi mjini Brussels, Ubelgiji wakati akipatiwa matibabu.

Kupitia wavuti wa MONUSCO, Bwana Sidikou amesema ni huzuni kufuatia masiba huo, na kuelezea kutambua mchango muhimu wa wa kiongozi huyo katika kukuza demokrasia chini DRC .

Amewataka wadau wa siasa nchini humo, kumuenzi kiongozi huyo wa chama cha UDPS, kwa kutekeleza kikamilifu makubaliano ya kisiasa yaliyotiwa saini mnamo Disemba 31, 2016 chini ya upatanishi wa baraza la kitaifa la maaskofu la DRC, CENCO.

Mkuu huyo wa MONUSCO, ametoa wito wa utulivu kwa wadau wote wa kisiasa ili kuendeleza majadiliano ya kuwezesha taifa la uwazi, heshima na kisha uchaguzi wa amani.