Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IAEA inafanya kila iwezalo kukabili saratani Afrika-Amano

IAEA inafanya kila iwezalo kukabili saratani Afrika-Amano

Mkurugenzi mkuu wa shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA, Bwana Yukiya Amano amesema shirika hilo liko mstari wa mbele katika vita dhidi ya saratani hususani katika kuzisaidia nchi zinazoendelea.

Akizungumza katika tukio maalumu la IAEA kuadhimisha siku ya saratani ambayo kila mwaka huwa Februri 4, Bwana Amano amesema kuboresha fursa ya kupata matibabu ya saratani katika nchi zinazoendelea imekuwa kipaumbele chake tangu aliposhika hatamu za uongozi wa shirika hilo mwaka 2009.

Akitoa mfano wa Nigeria nchi yenye watu milini 173, ambapo maelfu hufa kila mwaka kutokana na saratani inayoweza kutibika au kuzuilika kama wangeishi kwenye nchi zilizo na vifaa na wataalamu wa kutosha ni jambo la kusikitisha na kuhuzunisha.

Ameongeza kuwa na hali hiyo inazikumba nchi nyingi za Afrika ambako asilimia 80 ya watu wote bilioni 1.2 hawana fursa ya matibabu ya mionzi na huduma zingine za saratani. Na hivyo ametoa ahadi.

(SAUTI YA YUKIYA AMANO)

“IAEA inafanya kila iwezalo kushughulikia mgogoro huu. Mtazamo wetu ni kufanya huduma ya mionzi na matibabu ya nyuklia kupatikana kwa wingi zaidi.”