Kilimo eneo la Olgilai, Arusha kitakausha chanzo cha maji- UNDP
Shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP nchini Tanzania limesema kuendelea kwa kasi kubwa ya shughuli za kibinadamu kwenye chanzo cha maji cha Olgilai mkoani Arusha ni tishio kwa mustakhbali wa upatikanaji wa maji kwa wakazi wa mji wa Arusha.
Mratibu wa UNDP anayehusika na mazingira, Clara Makenya amesema ingawa wananchi wanasema shughuli za kilimo kwenye miteremko ya chanzo hicho cha maji zimekuwa zinafanyika kwa zaidi ya miaka 100 sasa, bado idadi ya wakati huo haikuwa kubwa kama sasa akisema..
(Sauti ya Clara)
Amependekeza hatua za kuchukua kuwa ni pamoja na kuwatafutia wakazi hao wa Olgolia maeneo mengine ya kilimo na kwamba..
(Sauti ya Clara)