Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICJ yatupilia mbali ombi la Kenya kuhusu kesi yake na Somalia

ICJ yatupilia mbali ombi la Kenya kuhusu kesi yake na Somalia

Mahakama ya kimataifa ya haki ICJ leo imetupilia mbali madai ya Kenya ya kutaka kesi ilisowasilishwa na Somalia dhidi yake kuhusu ugomvi wa mpaka wa majini. Katika uamuzi wake mahakama hiyo imesema kuna haja ya kusikiliza madai ya Somalia kuhusu kesi ya mpaka wa majini iliyowasilishwa mwaka 2014 dhidi ya Kenya.

Somalia iliyoko Kaskazini mwa Kenya inatarajia kwamba mpaka wa majini usogezwe hatua kuanzia kwenye eneo linalokutanisha nchi hizo mbili mshazari hadi kusini, wakati Kenya ikidai kwamba mpaka uwe kwa mstari ulionyooka kuelekea Kaskazini na sio Kusini kama inavyotaka Somalia.

Baada ya Somalia kuwasilisha kesi hiyo ICJ, Kenya ikawasilisha kesi pia kupinga kesi ya Somalia ikitaka ifutwe, lakini leo mahakama ya ICJ imetupiliwa mbali kesi ya Kenya.

Duru zinasema mpaka unaogombewa ni muhimu kwa sababu ya kusemekana kuwepo kwa mafuta na gesi katika eneo hilo.