Skip to main content

FAO yapatia wakulima nchini Iraq pembejeo za kilimo

FAO yapatia wakulima nchini Iraq pembejeo za kilimo

Zaidi ya wakulima 2000 walioathirika na vita nchini Iraq wamepokea tani 750 za mbolea kutoka shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO ili kuongeza uzalishaji wa mazao yao ya ngano katika majira ya baridi.

Mwakilishi wa FAO nchini Iraq Dkt Fadel El-Zubi, kila mkulima katika wilaya za Alqosh na Sheikan kwenye jimbo la Ninewa atapatiwa kilo 350 za mbolea, ambapo nusu ya kiwango hicho kitatumika sasa na kinachobakia kitatumika baadaye ili kuongeza ukuaji wa ngano.

Tangu mwaka wa 2014, kikundi cha kigaidi cha ISIL kilipochukua sehemu ya ukanda wa kilimo cha ngano, wakulima wamekuwa wakihaha kupata pembejeo za kilimo kama vile mbolea.

Wamekumbana na changamoto kama vile vikwazo vya kupata masoko, gharama kubwa ya pembejeo na hata kuchelewa kupatiwa malipo yao